Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Alex SandroChelseaJuventusT.ZTransfer ZoneUsajili Chelsea

Alex Sandro awaambia Juventus wamruhusu ajiunge na Chelsea.


Baada ya Chelsea kutuma ofa tatu zilizokataliwa na Juventus na mapema wiki iliyopita wakatuma ofa ya paundi milioni 60 ambayo Juventus walishindwa kuikataa ama kuikubali zaidi walisema wanasubiri maamuzi ya mchezaji mwenyewe,hatimaye beki Alex Sandro amewaambia Juventus wamruhusu kuondoka kwani anataka kucheza Chelsea msimu ujao. Alex Sandro atajiunga na Chelsea kwa ada ya paundi milioni 60 na kuvunja rekodi ya kua mchezaji ghali zaidi aliwahi kununuliwa na Chelsea ambayo sasa hivi inashikiliwa na Fernando Torres aliyesajiliwa kwa ada ya paundi milioni 50 akitokea Liverpool.Kama Sandro usajili wa Sandro utakamilika utakua ushindi mkubwa kwa Chelsea kwani wanajaribu kuziimarisha sehemu zote ambazo zilikua hazina wachezaji wa kipaji cha juu ili kuweza kupokezana.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib