Climb the mountains
Chelseachelsea tanzaniaManchester unitedManchester united to sign MaticNemanja maticT.ZTransfer ZoneUsajili ulaya
Nemanja Matic kujiunga Manchester United kwa ada ya paundi milioni 40.
Kutokana na habari iliyochapishwa na mtandao wa ESPN zikiseama kiungo wa Chelsea Nemanja Matic anategemea kujiunga na klabu ya Manchester United kwa ada ya paundi milioni 40 na usajili wake unatazamiwa kukamilika kabla ya mwisho wa wiki hii,Matic aliyejiunga na Chelsea kwa mara ya pili akitokea Benefica ya Ureno kwa ada ya paundi milioni 21 alikua na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Chelsea hasa msimu wake wa kwanza na kuweza kuisaidia klabu hiyo kushinda kombe la ligi kuu. Hata hivyo habari ilikua tofauti tangu Antonio Conte aanze kuifundisha Chelsea alikua akimuweka Matic benchi katika mechi nyingi japo alifanya vizuri katika mechi alizompa nafasi.Hii itakua ni habari ya kusikitisha kwa mashabiki wengi wa Chelsea ila tunamsukuru Nemanja Matic kwa kuitumikia klabu yetu tutakumbuka mchezo wake wa nguvu bila kuchoka na msimu aliotuwezesha kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment