Msimu huu umewafanya washumbuliaji kua wachezaji wanaowindwa zaidi katika dirisha la usajil huku washambuliaji kama Lukaku,Morata,Belloti na Griezman wakitajwa kua ndio wachezaji wanaohitajika zaidi na klabu kubwa barani ulaya huku baadhi ya klabu zikitaka kuwasajili washmabuliaji wawili kati ya ho waliotajwa hapo juu. Kitendo cha washambuliaji kuhitajika sana kwenye dirisha hili la usajili kimeifanya klabu ya Chelsea ispoteze muda katika kusaka mshambuliaji kwani tayari kamati ya usajili ya klabu Chelsea imeshakutana na aliyewahi kua mchezaji wao Romelu Lukaku,Chelsea wanataka kumshawishi mchezaji huyo akubali kujiunga na klabu ya Chelsea kwa mara ya pili. Hata hivyo uhamisho huo hautakua rahisi kwani watatakiwa kushindana na klabu ya Manchester United na pia watatakiwa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kitachovunja rekodi ya klabu ambacho kwa sasa ni paundi milioni 50 zlizotumka kumsajili Torres.
No comments:
Post a Comment