Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaDirisha la usajiliManchester CitySouthamptonVirgil Van Dijk

Licha ya Chelsea kumfukuzia muda mrefu ila Manchester City wapewa kipaumbele kumsajili Virgil Van Dijk


Beki wa Southampton Virgil Van Dijik alikua anatajwa kama mrithi wa John Terry Chelsea na klabu ya Chelsea ilianza kumfuatilia tangu mwanzo wa msimu, ila kikwazo kimeibuka baada ya klabu ya Southampton kusema wanataka walipwe kiasi cha paundi milioni 70 ili kumuachia beki huyo anayegombewa zaidi msimu huu. Klabu ya Chelsea ilikua tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 50 tuu,klabu ya Manchester City wao wameweka mezani kiasi cha paundi milioni 60 wakiwashinda Chelsea na Liverpool. Pamoja na kuandaa kiasi hicho kikubwa cha pesa lakini Man City wamemuandalia nyota huyo mshahara wa paundi laki 2 kwa wiki na endapo atakubali kujiunga nao atakua ndiye beki anayelipwa kiasi kikubwa cha pesa.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib