Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Alex SandroChelseaConteJuventusMarotta

Conte akomaa na Alex Sandro atuma ofa nyingine ya nne baada ya ofa tatu za mwanzo kukataliwa,Sasa Juve wamesema Sandro achague kubaki au kuondoka.


Katika orodha ya wachezaji ambao Antonio Conte aliikabidhi kwa kamati ya usajili ya Chelsea Alex Sandro ni moja ya wachezaji aliosisitiza klabu iwanunue,Chelsea walituma ofa tatu kuomba kumsajili mchezaji huyo lakini ofa zote hizo zilikataliwa na sasa wametuma ofa mpya ambayo inakadiriwa kufika paundi milioni 60 kuhakikisha wananasa nyota huyo. Mkurugenzi wa Juventus Beppe Matotta alidhibitisha kua wamepokea ofa kubwa ya mchezaji huyo ila bado hawajaamua,alisema hawatapenda kumuona mchezaji huyo anaondoka ila hawatamzuia. Marotta alisema kwa sasa ni juu ya Sandro yeye mwenyewe ikiwa ataomba kuondoka na kujiunga na Chelsea basi hatutakataa. Chelsea wanataka kumsajili nyota huyo kuongeza ushindani katika nafasi ya beki wa kushoto na kuongeza idadi ya mabeki kwani Kurt Zouma anategea kuondoka kwa mkopo.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib