Climb the mountains
Antonio ConteAtletico MadridChelseaChinaDiego Costa
Diego Costa amesema Conte amemtumia ujumbe mfupi na kumwambia hayupo katika mipango yake msimu ujao hivyo atafute klabu nyingine.
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amewashtua mashabiki wa Chelsea baada ya kusema amepokea ujumbe wa simu (SMS) kutoka kwa kocha wa Chelsea Antonio Conte ambapo alimwambia hayupo kwenye mipango ya Kikosi chake msimu ujao hivyo akamtaka Mshambuliaji huyo kutafuta klabu nyingine atakayoichezea msimu ujao. Japo Diego Costa ameweka wazi kua angependa kurudi Atletico Madrid lakini atashindwa kwani klabu hiyo imefungiwa kusajili mchezaji yoyote mpaka dirisha la January,kama Costa ataamua kurudi Atletico itamlazimu kukaa nje miezi minne huku akisubiri adhabu ya Atletico imalizike. Pia Diego Costa alipata ofa kubwa kutoka China ambayo ingemfanya kua mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani hata hivyo nyota huyo hafikirii kwenda China kwa kua anataka kucheza ligi yenye ushindani ili aweze kupata nafasi ya kuitwa kwenye Kikosi cha Hispania kitachoshiriki kombe la Dunia.
Tags: Antonio Conte
, Atletico Madrid
, Chelsea
, China
, Diego Costa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment