Climb the mountains
ChelseaMitch BatshuayiMonacoSevillaWest Ham
Mitch Batshuayi : Msimu ujao ninataka kucheza kwani kombe la Dunia linakaribia.
Mshambuliaji wa Chelsea Mitch Batshuayi ambaye goli lake dhidi ya West Brom liliipa Chelsea ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza alifunguka na kusema msimu ujao hayuko tayari kukaa benchi. Akihojiwa na mwandishi wa habari aliulizwa msimu ujao upo tayari kuendelea kukaa benchi? Na alijibu kama ifuatavyo "Hapana, hapana, hapana sipo tayari kukaa benchi msimu ujao kwani kombe la Dunia linakaribia hivyo inabidi nicheze mechi nyingi nifunge magoli ili ndoto yangu ya kucheza kombe la Dunia itimie" Pia nyota huyo alisema hajutii kuikataa klabu ya West ham na kujiunga na klabu ya Chelsea, alisema yeye hana maamuzi hivyo anawasikiliza Chelsea watamuambia nini kama atapata muda mwingi wa kucheza au watamtoa kwa mkopo. Klabu kadhaa zimeanza kuonyesha nia ya kumtaka mchezaji huyo kwa mkopo huku West ham wakifanya mazungumzo na Chelsea kuona kama wataweza kuwakopesha mchezaji huyo. Klabu nyingine ambazo zimeonyesha nia ya kumtaka ni Monaco na Sevilla.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment