Climb the mountains
Ac MilanCostaDiego Costa kuondoka Chelsea
Mshahara wa Diego Costa wawakimbiza AC Milan.
Baada ya Conte kuweka wazi hana mpango na mshambuliaji Diego Costa msimu ujao klabu ya AC Milan ilamua kukutumia mwanya huo kujaribu kumsajili Diego Costa lakini kwa sasa inaonekana wameshindwa kwani wameshindwa kukubaliana na kiasi cha mshahara anachotaka Costa. Wakala wa Diego Costa Jorge Mendes alikutana na bodi ya usajili ya AC Milan na kuwaeleza kua mteja wake anataka mshahara wa paundi laki 2 kwa wiki ili ajiunge nao kiasi ambacho AC Milan waliona ni kikubwa sana kwao. Pia AC Milan wameonyesha nia ya kumsajili Costa kwa mkopo lakini Chelsea wanataka kumuuza mchezaji huyo moja kwa moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)



No comments:
Post a Comment