Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

ChelseaNewcastleswanseaTammy Abraham

Swansea wawazidi ujanja Newcastle wamsajili Tammy Abraham kwa mkopo.


Wiki mbili zilizopita klabu ya Newcastle ilikua imeibuka kifua mbele kwenye mbio za kumsajili kinda machachali wa Chelsea Tammy Abraham kwa mkopo hata hivyo wakati wakifanya mazungumzo binafsi na mchezaji klabu ya Swansea nayo iliowaomba Chelsea kumchukua nyota huyo kwa mkopo baada ya Chelsea kukubali ombi la Swansea waliwaruhusu kufanya mazungumzo na kinda huyo. Baada ya Chelsea kukubali maombi ya timu zote mbili yani Newcastle na Swansea chaguo lilibaki kwa Tammy Abraham yeye mwenyewe kuchagua ni klabu ipi anataka kuitumikia msimu ujao,baada ya mazungumzo na pande mbili kinda huyo ameamua kujiunga kwa mkopo na klabu ya Swansea. Chelsea wameamua kumtoa nyota huyo kwenye klabu inayoshiriki ligi kuu ili apate uzoefu zaidi.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib