Wakati ligi nyingi zikimalizika na wachezaji kujiunga na timu zao za taifa na wengine kurejea kwao kwa ajili ya mapumziko. Ila jana ni tofauti kwa aliyekuwa mchezaji nyota wa Ivory Cost na timu ya Newcastle ambaye hadi umauti unamkuta alikua kwenye klabu yake mpya ya Tyneside yenye makazi yake nchini China baada ya kuanguka ghafla akiwa mazoezini pamoja na kuwahishwa hospitalini lakini baada ya lisaa limoja alifariki.Tiote alijipatia umauurufu mkubwa akiichezea klabu ya Newcastle United aliyojiunga nayo mwaka 2010 na kuondoka mwaka huu (2017) mwezi wa pili kwenda China,akiwa Newcastle alifanikiwa kuchezea mechi 150. Wachezaji wengi duniani pamoja na klabu za Ulaya,Afrika na Asia zimetuma salamu za rambirambi kwa familia yake huku moja wa marafiki wake akiweka mawasiliano yao ya mwisho muda mfupi kabla hajafariki ambayo imewagusa watu wengi. Tiote amefariki akiwa na miaka 30,wiki hii mke wake anategea kujifungua mtoto wao wa tatu ila kwa bahati mbaya hataweza kumuona baba yake. Pumzika kwa Amani Tiote....




No comments:
Post a Comment