Climb the mountains
Antonio ConteAtletico MadridCesc FabregasChelseaDiego Costa
Diego Costa apiga picha akiwa batani na jezi ya Atletico Madrid amuambia Fabregas amfikishie salamu zake kwa Conte.
Wakati Chelsea wakiendelea na mazoezi ya mwanzo wa msimu bila kuwa na mshambuliaji wao Diego Costa aliyezuiwa kushiriki mazoezi hayo sababu kocha alishasema hamuhitaji tena katika kikosi chake msimu ujao,lakini hali ni tofauti kwa Costa mwenyewe ambaye aliweka video fupi kwenye mtandao wa Snapchat iliyomuonyesha akiwa nyumbani kwao Brazil akijirusha huku akiwa amevaa jezi ya Atletico Madrid na baada ya kiungo wa Chelsea kuonekana akiwa ni moja wa watazamaji wa video hiyo Costa alimuambia Fabregas ampe salamu nyingi kocha Antonio Conte.Chelsea wanajaribu kumuuza Diego Costa kabla msimu mpya haujaanza huku Costa yeye mwenyewe akikataa klabu kumuuza kwenda China akisisitiza klabu imuuze kwenda timu yake ya zamani Atletico Madrid.
Tags: Antonio Conte
, Atletico Madrid
, Cesc Fabregas
, Chelsea
, Diego Costa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment