Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Antonio ConteChelsea TrainningChelsea wakifanya mazoeziEden HazardFikayo TomoriMazoeziPre season

Eden Hazard aanza mazoezi mepesi wakati wachezaji wengine wakiendelea kujiandaa na mechi za kirafiki.


Wakati mazoezi ya mwanzo wa msimu yakiaanza kushika kasi mashabiki wa Chelsea wanasubiri kwa hamu kumuona nyota wao Eden Hazard akirudi uwanjani baada ya kupata majeraha akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye mechi za kufuzu kombe la dunia.Habari njema ni kwamba Eden Hazar ameshaanza mazoezi mepesi ya kukimbia kwenye mashine pamoja na mengine ya viungo ikiwa kama njia ya kuhakikisha hakosi mechi nyingi pindi msimu utakapoaanza kwani yeye ni moja wa nyota wanaotegemewa sana na Chelsea hasa kipindi hikiwatachoenda kujaribu kutetea taji lao la ligi kuu ya Uingereza. Wakati Eden Hazard akiaanza mazoezi ya peke yake wachezaji wengine walionekana kwenye uwanja wa mazoezi wakiendelea kujifua huku Antonio Conte akiangalia kwa umakini mkubwa sana vijana wake wanavyojifua
Antonio Conte akifuatilia kwa karibu wachezaji wanavyofanya mazoezi.

Fikayo Tomori akikokota mpira ni moja ya makinda wachache aliebaki baada ya wengine kuuzwa na kutolewa kwa mkopo.

Makipa wao walikua wakifanya mazoezi ya peke yao walionekana wakicheza mchezo wa Volleyball.

Thibaut Courtouis akijaribu kuuwahi mpira.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib