Climb the mountains
Aston villaBakayokoChalobahChelsea wonderkidsJohn TerryMonaco WonderkidsMr.Chelsea
John Terry:Chelsea tuna makinda wenye vipaji vizuri kuliko wa Monaco kinachotakiwa ni kuwaamini na kuwapa nafasi.
Wakati akiwa amekamilisha usajili wa kujiunga na Aston Villa Legend wa Chelsea John Terry aliwapa somo klabu yake ya Chelsea kwa kuwaambia kua Chelsea ina vijana wenye vipaji vizuri sana kuliko hata makinda wa AS Monaco inachotakiwa ni Chelsea kuaamini na kuwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao uwanjani,alizungumza hivyo baada ya mjadala mkubwa kuibuka kuhusu usajili wa Bakayoko mwenye miaka 22 kusajiliwa na Chelsea wakati Chelsea wana kinda Nathanaiel Chalobah ambaye naye pia ana miaka 22 na anacheza nafasi sawa na Bakayoko. Terry alisema " Wakati mimi naanza kucheza nilipewa mechi tano au sita hivi lakini sikua tayari lakini kwa sasa tuna vijana wengi sana hapa Chelsea ambao wapo tayari na wanahitaji kupewa nafasi tuu Mashabiki wengine waliona ni bora Chelsea ingemuamini Chalobah na kumpa nafasi hiyo kwani ana umri sawa na Bakayoko na ameshacheza mechi za ligi kuu ya Uingereza huku wengine wakiona ni sawa Chelsea kumsajili Bakayoko kwa kua ana uzoefu na ligi ya mabingwa ya ulaya. Monaco imefanya vizuri msimu huu kwa kutumia wachezaji vijana zaidi katika kikosi chao kama Mbappe,Thomas Lemar na Bakayoko.
Tags: Aston villa
, Bakayoko
, Chalobah
, Chelsea wonderkids
, John Terry
, Monaco Wonderkids
, Mr.Chelsea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)




No comments:
Post a Comment