Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Alvaro MorataChelseaJames RodriguezMorata and RodriguezPerezreal madrid

Madrid wawaofa Morata na Rodriguez kwenda Chelsea kwa ada ya paundi milioni 133.


Rais wa Real Madrid Fiorentino Perez amewatumia Chelsea ofa ya kuwasajili nyota wake Morata na Rodriguez kwa ada ya paundi milioni 133 jumla. Chelsea ambao wapo sokoni wakitafuta mshambuliaji wa kuchukua mikoba ya Diego Costa kwa sasa wanafanya jitihada za kukamilisha usajili wa wachezaji wanaotakiwa na kocha wao mapema hasa baada ya kupata pigo kutoka kwa Lukaku baada ya nyota huyo kuamua kujiunga na Manchester United.Inasemekana Rais wa Real Madrid Perez hataki kuwauza nyota hao kwenda Manchester United baada ya kushindwana na klabu hiyo katika mazungumzo ya kumsajili kipa David De Gea. Chelsea walikaribia kumsajili Morata katika dirisha dogo la usajili mwezi wa kwanza lakini walijitoa baada ya Real Madrid kutaka kupewa kiasi cha paundi milioni 70 ili wamuuze nyota huyo,James Rodriguez naye amemuambia wakala wake amtafutie timu nyingine mapema kwani anataka kuondoka Madrid.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib