Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]


Klabu ya Chelsea imeanza mazungumzo na nyota wao Eden Hazard kuhusu kusajili mkataba mpya,klabu ya Chelsea imempa Eden Hazard mkataba wa paundi laki 3 kwa wiki ikiwa ni nyongeza ya paundi laki moja kutoka kwenye mkataba wake wa sasa ambao ni paundi laki 2.Klabu ya Chelsea inajitahidi kumshawishi nyota huyo kufuta mipango yake ya kwenda Real Madrid na kubakia klabuni hapo.Eden Hazard amekua na msimu mzuri licha ya timu kutokua na mwenendo mzuri msimu huu na amekua akihusishwa kuhamia klabu ya real Madrid msimu ujao ambayo pia imeonyesha nia ya kumtaka nyota huyo.Mara kadhaa nyota huyo amekua akisema kwenye vyombo vya habari kua ana furaha kua Chelsea na haoni sababu ya lazima kumfanya ahame ila taarifa kutoka kwa watu wakaribu zinasema nyota huyo ataangalia mkataba atakaopewa na Real Madrid kabla hajasaini mkataba wa Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib