
Shirikisho la mpira nchini Italy limemuweka kocha wa Chelsea Antonio Conte chaguo namba moja kuwa kocha mpya wa timu yao ya taifa. Timu ya taifa ya Italy haina kocha kwa sasa baada ya kumfukuza aliyekuwa kocha wao Gian Ventura baada ya kushindwa kufuzu kombe la Dunia ikiwa ni mara ya kwanza baada ya kushiriki kombe hilo kwa miaka 60.Makamu wa Rais wa shirikisho la soka nchini Italy Alessandro Costacurta alipoulizwa kuhusu hatma ya nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa alisema 'Bado sijaamua mpaka sasa ila nadhani Conte ni moja wa watakao weza kufanya vizuri,nitaongea naye miezi michache ijayo'. Wakati hayo yakiendelea hatma ya kocha huyo katika klabu ya Chelsea bado haieleweki kutokana na timu yake kutokua na matokeo ya kuridhisha msimu huu na mara kadha imekua ikisikia kua klabu ya Chelsea tayari imeanza kumtafuta mrithi wake huku aliyewahi kua kocha wa Barcelona Luis Enrique akihusishwa kuchukua nafasi yake msimu ujao. Conte amewahi kua kocha wa Italy kuanzia mwaka 2014-16 na baadae alitangaza atajiunga na Chelsea baada ya mashindano ya EURO kuisha.
No comments:
Post a Comment