
Wakati mashabiki wa Chelsea wakiwa bado wana majonzi ya kupoteza mechi na Man City wameongezewa habari ambayo sio njema masikioni mwao baada ya kufahamika kuwa Nyota wao Ngolo Kante alizimia mazoezini siku mbil kabla ya mechi ya Manchester City. Inaelezwa Kante alizimia wakati wakiwa katika vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kumaliza mazoezi na wachezaji wenzake jambo lililozua taharuki kwani walidhani amepatwa na mshtuko mkubwa wa moyo. Madaktari wa klabu waliwahi kwenda kumsaidia na baada ya vipimo waliona hana tatizo na walmruhusu kucheza Mechi dhidi ya City hata hivyo siku ya jumapili asubuhi Kante alianza kujisikia vibaya tena jambo lililopelekea klabu kuamua kumpuzisha ili kuepuka hatari kubwa zaidi. Hata hivyo inaelezwa Kante alifanya mazoezi jana na bila matatizo na anategemewa kucheza mechi ijayo dhidi ya Crystal Palace. Siku hizi kumekua na matukio ya mara kwa mara kwa wachezaji kupoteza maisha baada ya kuzimia na kupoteza maisha pindi wawapo mazoezini au hata wakati wa mechi.


No comments:
Post a Comment