Blog ikuleteayo habari mbali mbali kutoka klabu ya Chelsea kwa lugha ya kiswahili.

Climb the mountains

Post Page Advertisement [Top]

Alvaro MorataChelseaFA CupLeicester CityPedroSouthampton

Chelsea watinga nusu fainali FA Cup,wawaepuka mahasimu wake,wapangiwa droo nyepesi.


Klabu ya Chelsea imefanikiwa kutinga nusu fainali kombe la FA baada ya kuwatoa mabingwa wa zamani wa ligi ya Uingereza klabu ya Leicester City kwa jumla ya magoli mawili kwa moja magoli ya Chelsea yalifungwa na Alvaro Morata na goli la ushindi likifungwa na Pedro katika kipindi cha dakika 30 za ziada baada ya zile dakika 90 kumalizika matokeo yakiwa moja moja.Baada ya matokeo hayo droo ya nusu fainali ilipangwa huku Chelsea akipangiwa kucheza na Southampton akiwaepuka mahasimu wake Manchester United na Tottenham. Kwa droo hiyo klabu ya Chelsea inapewa nafasi zaidi kutinga fainali ikifanikiwa kuitoa klabu ya Southampton.Kocha wa Chelsea Antonio Conte aliweka wazi kua kwa sasa analiangalia kombe la FA kama kitu cha kuwafutia machozi mashabiki wa Chelsea msimu huu baada ya klabu hiyo kutokuwa na matokeo ya kulidhisha,Chelsea bado inapigana kuingia nne bora ili kupata nafasi ya kucheza UEFA msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]

| Designed by Colorlib